Akizungumza kabla ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa NATO huko Brussels, Kuleba alisema “hakuna sababu ya kuamini kuwa nchi za Magharibi zinakosa utashi wa kisiasa” kuongeza uwezo wa uzalishaji, lakini kuna taratibu za kiufundi nyingi ambazo lazima zifanyike kufikia lengo hilo.
Kuleba alisema siyo tu usalama wa Ukraine ambao uko hatarini katika vita hivi, lakini pia ulinzi na usalama wa eneo zima la Ulaya na Atlantik.
Alisema pia “hakuna kitakacho tuzuia” wakati Ukraine ikiwa imejikita katika lengo la kuhakikisha heshima ya nchi yake.
“Lazima tuendelee. Lazima tuendelee na mapigano,” Kuleba alisema. “Ukraine haitarudi nyuma.”
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg aliwaambia waandishi kuwa Russia inakabiliwa na shinikizo la kiuchumi, likiisukuma kuwa iitegemee zaidi China, na pia shinikizo la kijeshi ambalo inamaanisha kuwa iitegemee Korea Kaskazini na Iran kwa ajili ya silaha na vifaa.
Mkuu wa NATO alieleza hatua ya Ukraine kukamata tena asilimia 50 ya ardhi iliyokuwa imetekwa na Russia hapo awali katika vita, na pia vifaa na kusababisha hasara ya wafanyakazi kwa jeshi la Russia.
Lakini pia alitahadharisha dhidi ya kuikadiria kwa kiwango cha chini Russia kwa kuwa Rais Vladimir Putin bado dhamiri yake ya vita iko palepale.
Baadhi ya taarifa katika habari hii zinatokana na mashirika ya habari ya Agence France-Presse na Reuters.
Mwisho…
Forum