Pande hizo mbili zilipinga ufanisi wa shambulizi hilo, ambalo lilmefanyika siku mbili baada ya kuripotiwa kuwa Rais Joe Biden, amebadilisha sera ya Marekani na kuidhinisha matumizi ya makombora ya masafa marefu huku uvamizi wa Russia, nchini Ukraine ukifikia ya siku 1,000.
Maafisa wawili wa Marekani wameithibitishia VOA Jumanne kwamba sera inayokataza raia wa Ukraine kutumia silaha za masafa marefu zinazotolewa na Marekani kushambulia maeneo ya kijeshi ndani ya Russia imebadilika.
Naibu msemaji wa Pentagon, Sabrina Singh, Jumatatu alikataa kuthibitisha mabadiliko hayo, huku akiongeza kuwa Moscow haina sababu za kulalamika.
Forum