Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 12:28

Ukraine yasema kombora la Russia laua raia na kujeruhi


Maafisa wa Ukraine, Jumanne wamesema kombora la Russia lilishambulia mji wa Kramatorsk, na kuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine watatu.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, aliandika kwenye Telegram kwamba kombora hilo lilipiga katikati mwa jiji na kuharibu majengo ya ghorofa.

Amesema taifa la kishetani linaendelea kupigana dhidi ya raia, na kuharibu maisha na pamoja na yote ya kibinadamu.

Kila shambulizi linalo chukuwa maisha ya wasiokuwa na hatia litachukuliwa kisheria na kupata hukumu ya kusababisha mauaji, aliongeza kusema rais Zelenskyy.

Shambulio hilo limefanyika wakati Russia ikiashiria kile ilichosema ni kukataa kwa Ukraine kushiriki katika mazungumzo ya amani. Msemaji wa rais wa Russia, Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari kwamba Russia ina njia ya kijeshi tu nchini Ukraine.

XS
SM
MD
LG