Mtu mmoja amekufa na wengine wawili wamejeruhiwa na makombora ya Russia ambayo yamepita na kupiga katika jengo la kiwanda kusini mwa mji wa Odesa , hiyo ni kwa mujibu wa Serhiy Bratchuk , msemaji wa utawala wa kijeshi wa eneo hilo.
Licha ya mashambulizi ya anga ya Russia , China imesema mjumbe wake maalumu alikutana na rais Volodymir Zelensky wakati wa mazungumzo huko Kyiv mapema wiki hii na mwanadiplomasia mkuu wa ukraine.
Msemaji Wang Wenbin alisema alhamisi kwamba pande zinazogombana inabidi ziwe katika hali ya kuaminiana ili hatua za maendeleo zipigwe.
Ofisi ya rais wa ukraine imesema , maafisa wa nchi hiyo wakati wa mazungumzo walitaka kupata uungwaji mkono wa China kwa ajili ya kuisaidia Kyiv katika mpango wa amani. Pendekezo la zelensky ni pamoja na kurejeshwa kwa uadilifu wa eneo la nchi yake, kuondolewa vikosi vya Russia na kumuwajibisha rais wa Russia Vladmir Putin kisheria kutokana na uvamizi wa february 2022.