Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 09:45

Ukraine yakaribia kujiunga Jumuiya ya Ulaya


Ukraine na Tume ya Ulaya hivi karibuni zitatathmini maendeleo ambayo Kyiv imepata katika kuoanisha sheria yake na ile ya Umoja wa Ulaya na kuweka mfumo wa mazungumzo ya kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Mazungumzo hayo yanayotarajiwa kufanyika mwakani, rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, amesema katika hotuba yake ya kila siku Jumapili.

“Katika siku zijazo, pamoja na Tume ya Ulaya, tutazindua rasmi mchakato wa kutathmini sheria za Ukraine kwa kufuata sheria za EU,” Zelenskyy amesema.

Tume ya Ulaya mwezi uliopita iliripoti kwamba Ukraine, imetimiza mapendekezo manne kati ya saba ya mazungumzo ya kujiunga na Umoja wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na kuajiri maafisa wa kupambana na rushwa, kuandaa mahakama kwa ajili ya marekebisho makubwa na kuoanisha sheria ya vyombo vya habari kwa viwango vya EU.

Forum

XS
SM
MD
LG