Kuvamia kwa Kyiv katika eneo la Kursk la Russia, kunabadilisha mwelekeo wa vita na kuongeza ari kati ya wakazi waliochoshwa na vita kwa Ukraine, ingawa hatma ya uvamizi huo ambao ni shambulizi la kwanza dhidi ya Russia, toka vita vya pili vya dunia haijulikani.
Licha ya Ukraine kujipongeza kwa mafanikio yake ndani ya Russia, msukumo wa Russia, mashariki mwa Ukraine uko tayari kuchukuwa sehemu nyingine muhimu ya mji wa Pokrovsk.
Mashambulizi ya Ukraine kwenye madaraja matatu juu ya Mto Seym, yanaweza kuzuia vikosi vya Russia kuvuka mto huo, Ukraine kusonga mbele kwenye mpaka wake.
Tayari wanaonekana kupunguza kasi ya majibu ya Russia kwaa uvamizi wa Kursk, ambao Ukraine iliuanzisha Agosti 6.
Forum