Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 12, 2025 Local time: 08:22

Ukraine yadai kutungua "Drone" za Russia


Jeshi la Ukraine leo limesema mfumo wake wa ulinzi wa  anga umetungua ndege zisizo na rubani 25 kati ya 33 ambazo Russia imezitumia kushambulia mikoa ya Sumy na Odesa nyakati za usiku.

Oleh Kiper, Gavana wa Odesa, amesema shambulizi lilipiga eneo la Izmail kwa mara ya nne ndani ya siku tano na kumjeruhi mtu mmoja.

Ameongeza kusema pia shambulizi liliharibu miundombinu ya bandari, na jengo la utawala. Wizara ya ulinzi ya Russia imesema imeharibu ndege mbili zisizokuwa na rubani za Ukraine katika mkoa wa Rostov pamoja na Bryansk, na nyingine katika vitongoji vya Moscow.

Meya wa Moscow, Sergei Sobyanin amesema kupitia Telegragram kwamba mabaki ya ndege isiyo na rubani iliyotunguliwa yaliangukia katika wilaya ya Ramensky na hayakufanya uharibifu ama kusababisha vifo.

Forum

XS
SM
MD
LG