Luteni Jenerali Igor Kirillov, mkuu wa vikosi vya kijeshi vya kulinda nyuklia, kibaolojia na kemikali, aliuwawa alipokuwa anakwenda ofisini kwake, pamoja na msaidizi wake.
Nchi kadhaa, ikiwa pamoja na Uingereza na Canada, zilimuwekea vikwazo Jenerali Kirillov, mwenye umri wa miaka 54, kwa majukumu yake katika vita vya karibu miaka mitatu vya Moscow na Ukraine.
Hapo Jumatatu, Idara ya Usalama ya Ukraine (SBU), ilifungua uchunguzi wa uhalifu dhidi yake, ikimtuhumu kwa kuelekeza matumizi ya silaha za kemikali zilizopigwa marufuku. Afisa wa SBU, akizungumza kwa masharti ya kutotambulishwa kwa sababu hajaidhinishwa kutoa habari hiyo, amesema idara hiyo ndiyo imehusika na shambulizi hilo.
Afisa huyo alimtaja Jenerali Kirillov kuwa ni mhalifu wa kivita.
Forum