Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 01:11

Ukraine na Russia zadaiwa kupoteza wanajeshi wengi vitani muda huu


Wizara ya ulinzi ya Uingereza, Jumapili imesema  katika taarifa zake za kijasusi za kila siku kuhusu uvamizi wa Russia, nchini Ukraine kwamba pande zote mbili zimekabiliwa na vifo vingi katika maeneo ya kusini.

Russia inaelezwa kupoteza wanajeshi wengi zaidi toka mapambano makali yalipo fikiwa mjini Bakhmut mwezi Machi.

Hayo yakiendelea, Kremlin, Jumamosi imesema kwamba hakuna nafasi ya kuongeza muda mpango uliofikiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki wa Black Sea, unaoruhusu Ukraine, kusafirisha kwa usalama nafaka katika sehemu ya bahari inayo dhibitiwa na Russia.

Katika taarifa nyingine kuhusu vita vya Ukraine na Russia, gazeti la New York Times limeripoti kwamba kuna uwezekano kuliwekwa mlipuko iliyotegwa katika bwawa la Ukraine, la Khakhovka na kusababisha kuvunjika.

Taarifa hiyo ya New York Times, iliangazia maoni ya kitaalamu ya wahandisi wawili wa Kimarekani wanaofahamu kuhusu milipiko inavyoweza kuharibu vitu kama vile mabwawa.

Forum

XS
SM
MD
LG