Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 14:30

Ukraine na Russia zaanza tena mazumgumzo ya amani


Wakimbizi wanaokimbia vita nchini Ukraine, wakipiga foleni kwenye mpaka wa Medyka, wakivuka kuelekea Poland. Machi 10, 2022. Picha ya AP

Ujumbe wa Ukraine na Russia umeanza tena mazungumzo ya amani Jumatatu, siku moja baada ya Rashia kufanya shambulio baya la kombora kwenye kambi ya kijeshi magharibi mwa Ukraine, kilomita 25 tu kutoka Poland, mwanachama wa NATO.

Watu 35 waliuawa na wengine 134 kujeruhiwa katika shambulio hilo kwenye kituo cha kimataifa kwa ajili ya kulinda amani na usalama.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema Jumapili katika hotuba yake kwamba siku hiyo ilikuwa nyeusi kwa nchi yake kwasababu ya shambulio hilo, na pia alitoa onyo la wazi kwa viongozi wa nchi za magharibi kuhusu uwezekano wa shambulio kwenye kituo ambako vikosi vya NATO vinafanya mazoezi na wanajeshi wa Ukraine.

Rais Zelensky alisema Jumapili kwamba amejaribu kupanga mkutano na Putin, lakini hakufanikiwa ingawa wajumbe wa Ukraine na Rashia wanazungumza kila siku kuweka mipango ya kufunguwa njia salama kwa wanaokimbia vita na kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.

XS
SM
MD
LG