Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 23:50

Ukraine na China zajadili uvamizi wa Russia


Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba amejadili njia za kuzuia uvamizi wa Russia wakati wa mazungumzo na mwakilishi wa China Li Hui, serekali ya Ukraine imesema.

Wakati hayo yakielezwa, rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy anasema kwamba mashambulizi ya Russia yameua mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka mitano mjini Kherson.

Kwa upande wake White House inasema kuhusiana na mgogoro wa Ukraine na Russia, viongozi wa kundi la mataifa saba yenye uchumi mkubwa G7, wanaokutana Hiroshima, Japan baadaye wiki hii wanatarajiwa kuzungumza na rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy.

Wakati huo huo afisa wa ngazi ya juu wa ulinzi na afisa wa jeshi wameieleza VOA, kwamba Marekani imehesabu kwa makosa idadi ya misaada ya kijeshi iliyotowa kwa Ukraine, kwa zaidi ya dola bilioni tatu, ikiwa ni makosa katika hesabu zake na hivyo itaondoa wasiwasi uliyopo kwa utawala wa Marekani kuomba bunge fedha zaidi kuisaidia Kyiv katika mapambano.

XS
SM
MD
LG