Ukraine imesema Jumatatu kuwa ililipua daraja la reli katika mkoa wa Samara, kusini magharibi mwa Russia. Idara ya ujasusi ya jeshi la Ukraine imesema shambulio hilo lililenga uungaji mkono juu ya mto Chapaevka.
Shirika hilo limesema Russia ililitumia daraja hilo kusafirisha mizigo ya kijeshi. Kampuni ya reli ya Russia iliripoti tukio katika mkoa wa Samara, ikisema hakuna vifo lakini huduma hiyo imesimamishwa katika eneo hilo.
Wakati huo huo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ametoa wito kwa mataifa ya magharibi kutoa msaada uliocheleweshwa kwa Ukraine ambayo inajitetea dhidi ya mashambulizi ya Russia licha ya upungufu wa risasi.
Kama hili halitatokea, itakuwa moja ya kurasa za aibu zaidi katika historia, kama Marekani au Ulaya zitashindwa na ndege zisizo na rubani za Iran au ndege za kivita za Russia. Uovu wa Russia haupaswi kutiwa moyo na maamuzi dhaifu, ucheleweshaji wa kupeleka vifaa au kusita, alisema, akimaanisha mfuko wa misaada wa Marekani uliokwama kwa Ukraine kutokana na mvutano wa kisiasa katika Bunge la Marekani.
Forum