Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 27, 2023 Local time: 22:17

Ukraine imetungua ndege yake isiyokuwa na rubani


Moshi ukipaa angani katika mji wa Kyiv baada ya wanajeshi wa Ukraine kutungua ndege yao isiyokuwa na rubani iliyokumbwa na hitilafu za mitambo. May 4, 2023 PICHA: Reuters

Jeshi la Ukraine limeitungua ndege yake moja isiyokuwa na rubani, ambayo ilikumbwa na hitilafu za mitambo.

Ndege hiyo ilikuwa ikipaa katikati ya mji wa Kyiv, Alhamisi jioni.

Ripoti za awali kutoka kwa maafisa wa serikali zilisema kwamba Bayraktar TB2 ilikuwa imerushwa na adui, lakini baadaye jeshi likasema kwamba ilikuwa ya Ukraine.

Jeshi la anga la Ukraine limesema kwamba kuwepo angani kwa ndege hiyo isiyokuwa na rubani kungesababisha matatizo makubwa.

Hakuna ripoti za majeruhi wakati ndege hiyo isiyokuwa na rubani ilipoangushwa.

Akizungumza wakati alipoitembelea mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hana shaka kwamba rais wa Russia Vladimir Putin atakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine.

XS
SM
MD
LG