Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 22:48

Ukraine imetangaza siku ya maombolezo kufuatia shambulizi la Russia


Shambulizi la kombora limepiga kwenye mkoa wa Odesa huko kusini mwa Ukraine.
Shambulizi la kombora limepiga kwenye mkoa wa Odesa huko kusini mwa Ukraine.

Gavana Oleh Kiper alisema shambulio hilo la Russia lilipiga moja ya maeneo maarufu mjini Odesa ambapo watalii huenda kutembea

Gavana wa mkoa wa kusini mwa Ukraine wa Odesa ametangaza siku ya maombolezo leo Jumanne kufuatia shambulio la kombora la Russia lililosababisha vifo vya watu wanne na kuwajeruhi wengine zaidi ya 20.

Gavana Oleh Kiper alisema shambulio hilo la Russia lilipiga moja ya maeneo maarufu mjini Odesa ambapo wenyeji na watalii huenda kutembea na kwa michezo. Kiper alisema mtu wa tano alifariki baada ya kupata kiharusi kinachohusishwa na shambulio hilo.

Katika hotuba yake kwa njia ya video usiku wa Jumatatu, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alitoa rambirambi zake kwa familia za wale waliouawa na kusema majeruhi wanapatiwa huduma. Gavana wa mkoa wa Kharkiv nchini Ukraine amesema shambulizi la Russia katika mji mkuu wa mkoa huo liliua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Katika mji wa Dnipropetrovsk, gavana wa jimbo hilo alisema nyumba mbili ziliharibiwa na mashambulizi ya makombora ya Russia na ndege zisizo na rubani, lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa. Zelenskyy alisisitiza katika hotuba yake ya Jumatatu akitoa wito wake wa kupelekwa haraka silaha kutoka kwa washirika.

Forum

XS
SM
MD
LG