Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 05:47

Ukraine imeshambulia Russia kwa makombora


Mwnajeshi wa Ukraine akikagua mizinga ya Russia iliyoharibiwa July 21, 2023.
Mwnajeshi wa Ukraine akikagua mizinga ya Russia iliyoharibiwa July 21, 2023.

Jeshi la Ukraine limesema kwamba limekomboa kilomita 16 za mraba kutoka kwa wanajeshi wa Russia katika wiki moja iliyopita ya mapigano.

Ripoti hiyo inajiri wakati Russia imeripoti mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya Moscow na Crimea, iliyo chini ya udhibithi wa Russia.

Ukraine vile vile imesema kwamba Russia imetekeleza mashambulizi ya anga dhidi ya sehemu za kusini za bandari ya Odesa.

Jeshi la Russia limesema kwamba limeangusha ndege mbilizi zisizokuwa na rubani, zilizokuwa zimeulenga mji wa Moscow.

Meya wa Moscow Sergei Sobyanin, amesema kwamba mejengo mawili ambayo hayakai watu yaliharibiwa na hakuna ripoti za vifo.

Vyombo vya habari vya Russia vimeripoti kwamba mabaki ya ndege zisizokuwa na rubani yalipatikana Komsomolsky, karibu na wizara ya ulinzi.

Gavana wa Russia katika Crimea amesema kwamba ndege isiyokuwa na rubani ya Ukraine ilipiga gala la kuweka silaha, huku mfumo wa ulinzi ukiangusha ndege zingine zisizokuwa na rubani 11.

Forum

XS
SM
MD
LG