Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 13:15

Ukraine imeshambulia Russia


Moshi ukifuka baada ya ndege isiyokuwa na rubani ya Ukraine kushambulia kiwanda cha kusafisha mafuta, Ryazan, Russia. March 13, 2024.
Moshi ukifuka baada ya ndege isiyokuwa na rubani ya Ukraine kushambulia kiwanda cha kusafisha mafuta, Ryazan, Russia. March 13, 2024.

Zaidi ya ndege zisizokuwa na rubani 100 za Ukraine, zimeangushwa ndani ya Russia na kusababisha moto mkubwa msituni uliopelekea jumba kubwa la makao ya watu kuchomeka moto.

Shambulizi hilo limeripotiwa kuwa mojawapo ya mashambulizi makubwa kutekelezwa na Ukraine dhidi ya Russia, tangu Moscow ilipovamia Ukraine Februari 2022.

Wizara ya ulinzi ya Russia imeripoti kwamba imeangusha ndege zisizokuwa na rubani 125 katika maeneo saba, usiku wa kuamkia leo.

Ndege zisizokuwa na rubani 18 zimerushwa kuelekea eneo la Rostov na kusababisha moto msituni.

Raia 13 wamejeruhiwa katika mji wa Zaporizhzhia kusini mwa Ukraine, baada ya viongozi wa Ukraine kuonya kwamba Moscow ilikuwa inaandaa kwa mashambulizi mapta kudini mwa Ukraine.

Forum

XS
SM
MD
LG