Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 20:49

Ukraine: Hatuna wasiwasi na ripoti za Russia kupeleka silaha za Nyuklia Belarus


Rais wa Russia Vladimir Putin akifuatilia kwa njia ya video, hafla ya kuzindua ujenzi wa kinu cha Nyuklia cha Akkuyu, Uturuki. April 27, 2023
Rais wa Russia Vladimir Putin akifuatilia kwa njia ya video, hafla ya kuzindua ujenzi wa kinu cha Nyuklia cha Akkuyu, Uturuki. April 27, 2023

Afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Ukraine ameliambia shirika la utangazaji la BBC kwamba hana wasiwasi wowote kutokanaa na ripoti kwamba Russia imeanza kupeleka silaha zake za nyuklia nchini Belarus.

Katibu wa baraza la usalama wa taifa wa Ukraine, Oleksiy Danilov, amesema kwamba hatua hiyo si habari mpya .

Amesema kwamba Ukraine imejitayarisha kuanzisha mashambulizi yaliyotarajiwa kwa muda mrefu kukabiliana na uchokozi wa wanajeshi wa Russia nchini Ukraine.

Hata hivyo hajasema ni lini mashambulizi hayo yataanza, akisisitiza kwamba wana jukumu la kuilinda nchi yao.

Danilov amethibitisha kwamba kundi la mamluki la Wagner linaendelea kuwaondoa wapiganaji wake kutoka mji wa Bakhmut ambao umeharibiwa vibaya kutokana na vita hivyo.

Wizara ya ulinzi ya Uingereza vile vile imethibitisha katika taarifa zake za kila siku za ujasusi kwamba mamluki wa Wagner wameaanza kuondoka kuzunguka eneo la Donetsk katika mji wa Bakhmut.

Forum

XS
SM
MD
LG