Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:56

Ukraine haitashindwa na Russia, Biden asisitiza


Rais wa Marekani Joe Biden akitoa hotuba nje ya jumba la Royal Castle, Poland, Februari 21, 2023
Rais wa Marekani Joe Biden akitoa hotuba nje ya jumba la Royal Castle, Poland, Februari 21, 2023

Rais wa Marekani Joe Biden akiwa katika mji mkuu wa Poland Warsaw Jumanne usiku alitetea kwa nguvu juhudi za mwaka mzima za ushirikiano wa nchi za magharibi kuisaidia Ukraine kukabiliana na uvamizi wa Russia na kuapa kwamba ushirika huo hautakoma.

“Mwaka mmoja uliopita, dunia ilikuwa inaamini kwamba Kyiv itaanguka, Biden aliuambia umati wa zaidi ya Wapoland 10,000 waliokusanyika nje katika Jengo la Royal Castle.

“Kweli, nimetoka hivi punde kutembelea mji wa Kyiv, na ninaweza kuripoti kuwa Kyiv inasimama imara. Inasimama imara, na muhimu zaidi, inasimama huru.”

Biden ameahidi kwamba msaada kwa Ukraine hautasitishwa na NATO haitagawanyika.

“Ukraine kamwe haitashindwa na Russia,” alitangaza, akisema muungano huo una dhamira zaidi kuliko hapo awali, ya kuipa Ukraine zana na misaada ya kibinadamu kuisaidia kujihami dhidi ya Russia.

XS
SM
MD
LG