Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 19:05

Ukosefu wa vitambaa vya sodo ni kati ya sababu ya mimba za utotoni-"The Period Man"


James Atito maarufu kama The period man, ni mhasibu mkuu katika shirika la Stretchers Youth Organisation anatambulika kwa kampeni ya kukabiliana na dhana potovu kuhusu hedhi miongoni mwa wanaume huko Mombasa Kenya.
James Atito maarufu kama The period man, ni mhasibu mkuu katika shirika la Stretchers Youth Organisation anatambulika kwa kampeni ya kukabiliana na dhana potovu kuhusu hedhi miongoni mwa wanaume huko Mombasa Kenya.

Kukosekana kwa vitambaa vya sodo wakati wa hedhi na hivyo basi wengi huingia mtegoni na kujikuta kufanya ngono kupata sodo.

Wasichana walio balekhe hukabiliwa na changamoto nyingi ambazo huchangia wao kutomaliza masomo yao ama kuathiri afya yao ya kizazi.

Moja ni kukosekana kwa vitambaa vya sodo wakati wa hedhi na hivyo basi wengi huingia mtegoni na kujikuta kufanya ngono ili kupata sodo.

Ili kukabiliana na unyanyapaa miongoni mwa wasichana wakati wa hedhi, kijana anayejulikana kama "The period Man", anaendelea na kampeni ya kuhamasisha jamii kuhusu hedhi salama na vipi wasichana wanaweza kusaidiwa.

James Atito maarufu "The Period man", ni kijana anayetambulika kwa kampeni ya kukabiliana na dhana potovu kuhusu hedhi miongoni mwa wanaume. James ni mhasibu mkuu katika shirika la Stretchers Youth Organisation

Vijana wengine wakijishuhulisha na miradi inayopania kuleta faida ya kifedha, yeye amejishuhulisha na maswala ya usalama wa hedhi.

Mwanzoni ilikua kuzungumza na wanaume kuhusu na umuhimu wa wasichana kupata vifaa vya kujistiri , na baadae alipanua elimu hiyo kwa jamii kwa jumla.

Shuhuli hii ya maswala ya hedhi alianzisha mwaka 2019 , mara tu baada ya kurudi kutoka Turkana alikotumwa kuzungumzia maswala ya afya ya uzazi.

Japo fikra hizo zilianza mwaka 2016 alipohushuria kongamano la maswala ya hedhi salama wakati huo dada yake akiwa anaingia umri wa balekhe.

Katika hema kwa jina 'Makumbusho ya usafi wa hedhi', ndani yake kuna aina mbali mbali ya vifaa vya kujistiri wakati wa hedhi, na hata madaftari ya habari kuhusu hedhi.

Wanaume siku zote hujiepusha sana na maswala haya ya hedhi, na wasichana hutegemea mama kumzungumzia na kumsaidia.

Ila hilo halijamvunja moyo James, muhimu kwake ni kumaliza unyanyapaa na kumsaidia mtoto wa kike ili asikatishe ndoto za maisha yake kwa kukosa masomo sababu ya hedhi.

Ukosefu wa vitambaa vya sodo ni kati ya sababu za wasichana hasa katika maeneo ya mashambani kupata mimba za utotoni kutokana na ushawishi wa baadhi ya wanaume kwamba watawasaidia kupata bidhaa hizo muhimu.

Mbali na hamasa "The period man" pia husambaza vitambaa vya sodo kutoka kwa wafadhili.

Licha ya changamoto nyingi ikiwemo kufikia wasichana wote walio na mahitaji, mradi huu umekuwa wa mafanikio.

Kupitia wafadhili amefanikiwa kusambaza menstrual cups milioni 3 katika mataifa ya Afrika Mashariki na wamechangia kutengezwa kwa sera za serikali kuhusu usafi wa hedhi Kenya.

Imeandaliwa na Amina Chombo Mombasa Kenya.

XS
SM
MD
LG