Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 23:11

Ukosefu wa fedha watishia kambi ya Dadaab


Dola milioni 25 zinahitajika ili kuendeleza kutoa msaada kwa wakimbizi 465,000 waliopo huko

Makundi kadhaa ya kimataifa ya kutoa msaada yanayofanya kazi nchini Kenya yanaonya kuwa upungufu mkubwa wa fedha za msaada unatishia maelfu ya maisha ya watu katika kambi kubwa ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya.

Kundi hilo lenye mashirika nane ya kutoa msaada ikiwemo Oxfam na Save the Children lilisema katika taarifa yake kwamba dola milioni 25 zilihitajika ili kuendeleza kutoa msaada kwa watu 465,000 waliopo kwenye kambi ya Dadaab. Ilisema fedha za msaada kwa mahitaji muhimu zinatarajiwa kumalizika katika muda wa kipindi cha miezi miwili hadi mitatu.

Idadi ya wakimbizi katika kambi imeongezeka kupita kiasi katika kipindi cha mwaka uliopita japokuwa hali ya ukame katika eneo kwa kiasi fulani imeimarika. Lakini makundi ya kutoa msaada yanaonya kwamba fedha za msaada kutoka makundi ya kimataifa ya kutoa msaada kwenye kambi bado hazijafika.

Wakimbizi wengi katika kambi ya Dadaab ni wasomali ambao walikimbia nyumba zao kwa sababu ya mgogoro wa muda mrefu, umaskini na hali mbaya ya ukame iliyotokea mwaka jana.

XS
SM
MD
LG