Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 23:37

Uhaba wa chakula unatarajiwa kuongezeka Afrika


Mti wa Mhindi ukiwa umekauka kutokana na ukame.
Mti wa Mhindi ukiwa umekauka kutokana na ukame.

Watalaamu wa misaada wa kiafrika wanasema wana wasi wasi kuwa bara hilo ambalo linakumbwa na ukame huenda likawa nyuma ya mataifa yaliyokumbwa na mizozo kama vile Syria, Yemen na Iraq wakati maafisa wa kimataifa wa misaada wakikutana wiki hii kwa mara ya kwanza kuwahi kufanyika kwa mkutano wa viongozi kuhusu huduma za dharura unaofanyika mjini Istanbul.

Shadrack Omol mshauri mwandamizi katika idara ya mfuko wa dharura wa watoto katika Umoja wa Mataifa anasema mwanya wa kujibu kwa njia muafaka unajifunga haraka.

Wakulima wa mahindi eneo la Dowa nchini Malawi. Feb. 3, 2016.
Wakulima wa mahindi eneo la Dowa nchini Malawi. Feb. 3, 2016.

Mwenendo wa hali ya hewa ambao umepelekea ukame, maarufu kama el nino umelipiga eneo la mashariki na kusini mwa Afrika tangu mwaka 2015 kwanza hali hiyo ilijitokeza katika sehemu ambazo zimekuwa zikikumbwa na mafuriko mabaya na kuyafanya kuwa makavu kutokana na ukame mbaya sana.

Mzozo huu umeathiri kiasi cha watu milioni 32 kusini mwa Afrika peke yake na watalaamu wanasema wanatarajia tathmini mpya kubainisha ongezeko la mpaka karibu watu milioni 50 mwanzoni mwa mwezi June.

XS
SM
MD
LG