Msemaji wa ofisi ya rais wa Azerbaijan ameliambia shirika la habari la AFP kwamba “ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa uliwasili Karabakh Jumapili asubuhi, hasa kutathmini mahitaji ya kibinadamu.
Ni kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 30, ujumbe wa Umoja wa Mataifa kufika kwenye eneo hilo.
Waarmenian wanaotaka kujitenga, ambao walithibiti eneo hilo kwa miongo mitatu walikubali kuweka chini silaha, kuvunja serikali na kujiunga tena na jeshi la Azerbaijan kufuatia mashambulizi ya siku moja ya Azerbaijan wiki iliyopita.
Ufaransa iliikosoa Azerbaijan kwa kuruhusu tu Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa kuingia huko, baada ya karibu wakazi wote kukimbia.
Karibu wakazi wote wa Karabakh wanaokadiriwa kuwa sawa na 120,000 walikimbia eneo hilo katika siku zilizofuata, na kusababisha mzozo wa wakimbizi.
Forum