Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 03:32

Ujerumani yapiga kura kutambua mauaji ya Armenia


Wabunge wa Ugerumani wamepiga kura mapema leo ya kutambua mauwaji ya waarmenia wakati wa vita vya kwanza vya dunia na waturuki wa Ottoman kuwa ya jinai.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ameonya kuwa iwapo sheria hiyo itapitishwa, huenda ikaharibu uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi, kibiashara, kisiasa na hata wa kijeshi kati ya Ugerumani na Uturuki.

Armenia inasema kuwa watu milioni 1.5 waliuwawa kati ya 1915 na 1917. Uturuki inakubali kuwa maelfu ya waarmenia walikufa lakini imekanusha kuwa mauwaji hayo yalitokana na kampeni ya kijinai.

Ugerumani sasa inaungana na mataifa mengine 20 yalioorodhesha mauwaji hayo kuwa ya jinai.

XS
SM
MD
LG