Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 22:44

Ujerumani na Spain nguvu sawa


Mjerumani Niclas Fullkrug akisherehekea kufunga bao lake la kwanza na Jamal Musiala kwenye uwanja wa AlBayt aliposawazisha dhidi ya Spain. REUTERS
Mjerumani Niclas Fullkrug akisherehekea kufunga bao lake la kwanza na Jamal Musiala kwenye uwanja wa AlBayt aliposawazisha dhidi ya Spain. REUTERS

Timu za Ujerumani na Spain zimetoka sare ya bao 1-1 katika uwanja wa Al Bayt siku ya Jumapili.

Ujerumani sasa imerejesha matumaini yake ya kusonga mbele katika raundi ya pili baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Japan.

Matokeo hayo yamewapa mabingwa hao mara nne wa kombe la dunia pointi moja muhimu inayohitajika ili kusalia nchini Qatar, huku Uhispania wakiimarisha nafasi yao ya juu kwenye msimamo wa Kundi E kwa pointi nne.

Alikuwa ni Alvaro Morata alipiga mkwaju mkali na kuukwamisha mpira wavuni na kumpita kipa Manuel Neuer kufuatia krosi ya chini chini ya Jordi Alba katika dakika ya 62 na kuifanya Uhispania kuongoza.

Lakini wana wa Ujerumani walikuja juu na kusawazisha katika dakika ya 83 kuitia kwa Niclas Fullkrug.

Ujerumani itacheza na Costa Rica katika mechi ijayo na ya mwisho, ambayo pia iko kwenye kinyang'anyiro cha kutaka kusonga mbele baada ya ushindi wa kushangaza dhidi ya Japan na iko katika nafasi ya tatu wote wana pointi tatu lakini iko nyuma ya Japan kwa tofauti ya mabao.

Morocco yaangusha vigogo wa Belgium

Wawakilishi wengine wa Afrika Morocco wamewashtua Belgium na kuwaangusha miamba hao kwa bao 2-0 katika uwanja wa Al Thumama.

Walikuwa ni wachezaji Sabiri Abdelhamid katika dk 73 na Aboukhlal Zakaria katika dakika za majeruhi walizamisha jahazi la Belgium.

Morocco ambayo ina washabiki wengi katika michuano hii imepata uungaji mkono mkubwa na kujikuta kama wanacheza nyumbani.

Mchezaji wa Belgium Amadou Onana alipata kadi ya pili ya njano kunako dakika ya 28 kwa kufanya madhambi kwa mchezaji wa Morocco ikiwa na maana sasa atakosa mechi ijayo.

Beki hatari wa kulia wa Morocco ambaye anatajwa kama moja ya mabeki bora wa kulia duniani Achraf Hakimi anayechezea PSG ya Ufaransa alipanda kwa mashambulizi na kukosa goli la wazi kunako dakika ya 34 ya mchezo,

Hakim Ziyech aliweka mpira wa adhabu kimiani lakini goli lake lilikataliwa kwasababu wachezaji wawili wa Morocco walionekana kuotea.

Historia pia imeandikwa katika mchezo huu ambapo refa msaidizi alikuwa mwanamke wa kwanza refa katika mechi za wanaume nchini Japan Yoshimi Yamashata.

Na katika hali isiyo ya kawaida nahodha wa timu ya taifa ya Belgium Kevin De Bruyne amesema timu yake ina wachezaji wazee na haiwezi kuchukua kombe la dunia.

Costa Rica yaishangaza Japan

Nayo timu ya Costa Rica ilitunza heshima yake na kuwashangaza wajapan baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 katika uwanja wa Ahmad bin Ali mjini Doha Qatar.

Baada ya timu hiyo kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Spain kwa bao 7-0 iliingia uwanjani na nia moja ya kutunza heshima yake.

Costa Rica imekuwa timu ya kwanza kuruhusu mabao saba katika mchezo mmoja, kisha kushinda mechi iliyofuata kwenye Kombe la Dunia tangu Paraguay mwaka 1958 (ilipoteza 7-3 kwa Ufaransa, ikashinda 3-2 dhidi ya Scotland).

Timu hii ina wachezaji 6 walioshiriki kombe la Dunia mwaka 2014 na kufika hatua ya robo fainali kwa hiyo sio timu ya kubeza.

Washabiki wa Japan walikuwa wakipiga kelele kuonyeshwa kukasirishwa kwao na kukosa magoli huku mama mmoja mshabiki wa Costa Rica alionekana akifanya sala katika dakika za majeruhi za mchezo huo uliojaa ushindani mkali.

Costa Rica walipambana vikali katika mchezo huo na kumiliki mpira vyema katika kipindi cha kwanza na kipindi cha pili chote Japan walimiliki mpira lakini ngome ya Costa Rica ilikuwa imara .

Bao pekee la Costa Rica ambalo sasa linaipa pointi tatu timu hiyo na kuwa na nafasi ya kusonga mbele lilifungwa na Fuller Keysher katika dakika ya 81.

Croatia yaichakaza Canada

Na timu ya taifa ya Canada sasa imeaga rasmi michuano ya kombe la dunia baada ya kucpoteza wa pili mfulululizo dhidi ya Croatia kwa jumla ya mabao 4-1.

Croatia ilithibitisha kwamba ina uzoefu mkubwa baada ya kuichabanga timu hiyo ya Canada anbayo imerudi kucheza kombe la dunia baada ya miaka 34 katika uwanja wa kimataifa wa Khalifa.

Canada walikuwa wa kwanza kupachika bao mapema kabisa katika mchezo huo kunako dakika ya pili kupitia kwa mchezaji wao machachari Alphonso Davies.

Nao Croatia walisawasisha muda mfupi kabla ya mapumziko katika dakika ya 44 kupitia kwa Marko Livaja.

Na katika kipindi cha pili Canada waliendelea kushambulia lakini bila kupata magoli na hatimaye Croatia walionyesha uzoefu wao kwa kuongeza mabao mengne matatu yaliofungwa na Kramaric Andrej katika dakia ya 36 na akaongeza tena jingine katika dakika ya 70 na bao la nne na la mwisho lilipachikwa nyavuni na Lovro Majer baada ya dakika 90 kumalizikia ndani ya dakika za majeruhi.

Kwa maana hiyo timu za Croatia, Morocco,Japan, Spain, Ujerumani, Costa Rica bado zina nafasi ya kusonga mbele.

XS
SM
MD
LG