Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 16:55

Mshukiwa wa shambulizi la Berlin auawa Milan, Italy


Waziri wa mambo ya ndani wa Italy, Marco Minniti (kushoto) na mkuu wa Polisi Franco Gabrielli wakiongea na waandishi wa habari mjini Rome.

Soko la krismas mjini Berlin limefunguliwa huku kukiwa na ulinzi mkali na vizuizi kuzunguka eneo hilo.

Maafisa wa Italy wanasema raia wa Tunisia anayeshukiwa kuendesha shambulizi katika soko la krismas mjini Berlin alipigwa risasi na polisi katika kituo cha treni mjini Milan Ijumaa asubuhi.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Marco Minniti wakati anazungumza na vyombo vya habari Ijumaa, amesema polisi walikuwa hawana shaka kwamba mtu aliyeuwawa wakati akipambana kwa risasi na polisi alikuwa ni Anis Amri, mtuhumiwa namba moja katika shambulizi la soko la Ujerumani siku ya Jumatatu.

Polisi wameeleza kuwa Mtunisia huyo mwenye umri wa miaka 24 alisimamishwa na walinzi wa doria karibu na kituo cha stesheni ya treni huko Sesto San Giovanni, nje ya mji wa Milan, mapema Ijumaa. Ripoti ya polisi imeeleza kuwa mshukiwa huyo alichomoa silaha alipotakiwa kuonyesha kitambulisho, na kumpiga risasi na kumjeruhi afisa wa polisi.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani, Tobias Plate amewaambia waandishi wa habari mjini Berlin, Ujerumani amepata faraja kwa habari za Amri kupigwa risasi. “Kuna kila dalili kwamba huyu ndiye mtu hasa (anayetafutwa kuhusiana na shambulizi). Ikiwa hili litathibitishwa, wizara itapata ahueni kwamba mtu huyu hatokuwa tishio tena,” alisema.

Waandaaji wa sherehe hizi waliamua kufungua soko bila ya sherehe zozote kwa kutokuweka muziki au taa zenye mwanga mkali, na badala yake kumewekwa mishumaa na maua yaliyoachwa katika eneo hilo la shambulizi kama ni sehemu ya rambirambi za waliouwawa.

Mtuhumiwa mkuu katika shambulizi hili ni muomba hifadhi ya ukimbizi aliyekataliwa na kuwekwa katika darubini za polisi kufuatia fununu kwamba huenda alijaribu kununua silaha kufanya mashambulizi. Lakini uchunguzi huo ulisitishwa mwezi Septemba.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG