Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 11:51

Ujerumani inaunga mkono Afrika kuwa na mwanachama wa kudumu baraza la usalama UN


Rais wa Kenya Dr. William Ruto (kulia) akiwa na chansela wa Ujerumani Olaf Scholz (kushoto) wakihutubia waandishi wa habari katika ikulu ya rais Nairobi, Kenya. May 5, 2023
Rais wa Kenya Dr. William Ruto (kulia) akiwa na chansela wa Ujerumani Olaf Scholz (kushoto) wakihutubia waandishi wa habari katika ikulu ya rais Nairobi, Kenya. May 5, 2023

Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz, amesema kwamba Ujerumani inaunga mkono mpango wa bara la Afrika kuwa na uwakilishi wa kudumu kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Akiwa kwenye ziara nchini Kenya, Scholz amemueleza rais William Ruto kwamba anaamini kuwa matatizo ya Afrika yatasuluhishwa kwa uongozi wa nchi za Afrika, akitoa mfano wa mapigano yanayoendelea nchini Sudan.

Amesema kwamba Ujerumani inaunga mkono wazo la Afrika kuwa mwanachama wa kudumu kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa, paamoja na kupewa nafasi kwa umoja wa Afrika kuwa na mwakilishi kwenye kundi la nchi tajiri 20 duniani G-20.

Kwa sasa, bara la Afrika linawakilishwa na Gabon, Ghana na msumbiji kama wanachama wasio wa kudumu kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa.

XS
SM
MD
LG