Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:14

Ujerumani huenda ikaondoa vikosi vyake Mali


Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Christine Lambrecht
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Christine Lambrecht

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Christine Lambrecht amesema Jumapili kwamba ana wasiwasi iwapo taifa lake litaendelea kuweka vikosi vyake nchini Mali wakati hali ya taharuki ikiendelea kutanda kati ya taifa hilo na washirika wake wa kimataifa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Ujerumani ina takriban wanajeshi 1,200 nchini Mali wakiwa sehemu ya mpango wa miaka 9 wa kuweka amani pamoja na kukabiliana na makundi ya kigaidi nchini humo.

Uhusiano wa Mali na washirika wake wa kimataifa ulianza kuyumba pale kundi la kijeshi lililochukua madaraka lilipokataa kuitisha uchaguzi baada ya kufanyika kwa mapinduzi ya serikali mara mbili, pamoja na kuletwa kwa mamluki wanaosemekana kutoka kampuni ya Wagner ya Russia.

Wakati akifanya mahojiano na shirika la habari la ZDF, Lambercht amesema kwamba anafikiri kwamba hawajakaribishwa tena nchini humo. Baadhi ya mataifa ya Ulaya yanadai kuwekewa masharti na utalwa wa Mali kuhusiana na operesheni dhidi ya ugaidi, wakati vikosi vya Denmark vikiamurishwa kuondoka nchini humo mwezi ulioyopita.

XS
SM
MD
LG