Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 23:56

Uingereza yakamilisha kilele cha sherehe za utawala wa Malkia


Wakazi wa London wafurahia sherehe hizi huku baadhi wakikerwa na ufujaji wa fedha za umma uliohusishwa na familia ya kifalme

Maelfu ya wakazi wa jiji la London walihudhuria sherehe kubwa kwenye uwanja wa Kasri ya Buckingham, makazi rasmi ya Malkia, kwa siku ya mwisho ya sherehe za miaka 60 za utawala wa Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza.

Malkia Elizabeth mwenye umri wa miaka 86 na familia yake waliwapungia mikono wakazi wa London huku wakipeperusha bendera za nchi hiyo kutoka kwenye eneo la nje Jumanne wakati ndege ya kifalme ikiruka angani.Wakati huo huo Rais Barack Obama wa Marekani alitoa salamu binafsi kwa malkia akisema anamatumaini ataendelea kuongoza na kuwa na afya salama kwa miaka mingi ijayo. Katika video iliyotolewa kwenye tovuti ya White House bwana Obama alimuita malkia “living witness” kwa kuboresha uhusiano maalumu kati ya Uingereza na Marekani, dhamana ambayo alisema inabaki kuwa muhimu sana kwa nchi zao hizi mbili na dunia.

XS
SM
MD
LG