Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 03:17

Uingereza yakamilisha kabisa mchakato wa kuondoka umoja wa ulaya


Mkataba wa baada ya Uingereza kuondoka umoja wa ulaya unaanza kutumika leo alhamisi, baada ya kusainiwa na kuwa sheria.

Bunge la Uingereza liliunga mkono mkataba huo katika kikao cha haraka iliyofanyika jumatano, baada ya kupatikana mkesha wa Krisimasi.

Uingereza inaondoka soko la Pamoja la umoja wa ulaya na umoja wa forodha, lakini makubaliano hayo yanafikisha kikomo uwezekano wa kuweka ushuru kwa bidhaa.

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema kwamba hatma ya nchi hiyo kunwa sasa imo mikononi mwa waingereza.

Lakini wakosoaji wanasema Uingereza itakumbana na changamoto kadhaa kuliko jinsi ilivyokuwa wakati ni mwanachama wa umoja wa ulaya.

Uingereza ilijiondoa umoja wa ulaya Januari tarehe 31 mwaka huu, lakini ililazimika kuendelea kufuata sheria za biashara za umoja huo hadi sasa.

Mkataba huo unaoanza kutekelezwa miaka minne na nusu baada ya wapiga kura wa Uingereza kuamua kuondoka umoja wa ulaya, unaweka kanuni mpya za kibiashara na usalama.

"Ni vyema. Tunawashukuru sana, kila mtu. Nataka kila mtu kuelewa kwamba mkataba ambao nimesaini, sio mwisho bali ndio mwanzo. Na nadhani ni mwanzo wa uhusiano mzuri sana utakavyokuwa kati ya Uingereza na marafiki wetu katika umoja wa ulaya. Mkataba ndio huu. Najua swali mtakalokuwa mnajiuliza ni iwapo nimeusoma. Jibu ni kwamba, nimeusoma na ni mkataba mzuri sana kwa nchi hii. Na pia kwa marafiki na washirika wetu.” Amesema waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson.

XS
SM
MD
LG