Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 10:39

Uingereza yapiga kura kujitoa Umoja wa Ulaya


Kiongozi wa kampeni ya kujitoa Nigel Farage akishangilia kujitoa.

Uingereza imepiga kura kujitoa Umoja wa Ulaya utabiri unaonyesha ikiwa karibu kura zote zimekwishahesabiwa.

Shirika la habari la ITV NA Sky news huko Uingereza yote kwa pamoja yametangaza kambi ya kuondoka imeshinda ikiwa na karibu asilimia 52 ya kura.

Watu waliripotiwa kujitokeza kwa mwingi kupiga kura hiyo ambayo inagusa masuala ya uhamiaji uhuru , usalama na siku zijazo za uchumi wa Uingereza tume ya uchaguzi ya Uingereza imeeleza.

“Maafisa wa upigaji kura wamethibitisha kuwa jumla ya kura 33,568,184 zitajumuishwa katika kura ya maoni. Kwa mujibu wa watu waliojitokeza kupiga kura waliothibitishwa kuwa 46,500,001 , waliojitokeza kupiga kura walikuwa asilimia 72.2 tume hiyo ilisema katika taarifa yake.

Kiongozi wa kampeni ya kujitoa Nigel Farage amsema Juni 23 itakumbukwa kihistoria kama siku ya uhuru na kumtaka waziri mkuu David Cameron kujiuzulu.

Hatua hiyo imepelekea paundi ya Uingereza kuanguka vikali na ilikuwa imeenda chini zaidi ya asilimia tano katika usiku mmoja mjini London.

XS
SM
MD
LG