Mkutano huo umegubikwa na kuzomewa vikali kwa rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, na Rais wa Marekani, Donald Trump, kwa “kutoshukuru uungwaji mkono wa Marekani” katika vita vya Ukraine dhidi ya uvamizi wa Russia, wakati walipokutana Ijumaa katika White House.
Lakini Waziri Mkuu Starmer, amesema analenga kuwa daraja la kurejesha mazungumzo ya amani na alitumia kuvunjika kwa mazungumzo hayo kama fursa ya kuungana tena na Marais Trump na Zelenskyy pamoja na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron badala ya kuongeza mvutano.
Forum