Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 24, 2025 Local time: 00:01

Uingereza yaitoa Australia na kuingia fainali ya kombe la dunia la wanawake


Uingereza wakishangilia ushindi baada ya kuitoa Australia kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake Australia na New Zealand 2023.
Uingereza wakishangilia ushindi baada ya kuitoa Australia kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake Australia na New Zealand 2023.

Uingereza  sasa itamenyana na Uhispania katika fainali siku ya Jumapili.

Timu ya Uingereza - Lionnesses imeishinda Australia kwa jumla ya mabao 3-1 mjini Sydney Australia Jumanne na kutinga fainali yake ya kwanza kabisa ya Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake katika historia yao.

Nahodha wa Australia Samantha Kerr alifunga moja ya mabao bora zaidi ya michuano hiyo lakini haikutosha kwa wenyeji hao kwani wachezaji wa Uingereza Ella Toone, Lauren Hemp na Alessia Russo wote waliifungia mabao timu yao na kushinda mchezo huo.

Uingereza sasa itamenyana na Uhispania katika fainali siku ya Jumapili.

Uhispania wameingia fainali hizo baada ya kuwafunga Sweden bao 2-1.

Na pia Jumamosi kutakuwa na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya wenyeji Australia na Sweden.

Katika mechi hiyo Uingereza pia walikuwa vizuri mbele ya lango huku wakichukua nafasi zao kuhakikisha wanafunga mabao.

Uingereza sasa imepoteza mara moja pekee katika mechi 38 tangu kocha Wiegman achukue nafasi ya mikoba ya timu hiyo mwaka 2021, kipigo cha 2-0 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Australia mjini London na kumaliza msururu wa mechi 30 bila kufungwa.

Forum

XS
SM
MD
LG