Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 28, 2025 Local time: 19:20

Uingereza yahimiza utulivu Zimbabwe


Wakati wa sherehe za uhuru Aprili 18, 1980, akiwa Waziri Mkuu Robert Mugabe akiapishwa huko Highfields, Harare, Zimbabwe.
Wakati wa sherehe za uhuru Aprili 18, 1980, akiwa Waziri Mkuu Robert Mugabe akiapishwa huko Highfields, Harare, Zimbabwe.

Uingereza ambayo iliwahi kutawala lililokuwa koloni lake, Zimbabwe, imehimiza kuwepo utulivu kufuatia kile kinachoonekana kama ni hatua ya kuondolewa Rais Robert Mugabe kutoka kwenye madaraka.

Kiongozi wa zamani wa Zimbabwe aliyepigania uhuru wa Zimbabwe mwaka 1970, Mugabe, amekuwa na mahusiano yenye mvutano na Uingereza, jambo ambalo Marekani na Ushirika wa nchi za Ulaya wanamtuhumu kwa kuendesha uvunjifu wa haki za binadamu.

Nje ya Ubalozi wa Zimbabwe nchini Uingereza, sherehe zilianza mapema Jumatano katika duru za wanaounga mkono upinzani wakati dalili zilizojitokeza zikiashiria kumalizika utawala wa Mugabe.

“Hakika tunaridhia kile alichokifanya siku za nyuma. Lakini kwa bahati mbaya, hakuweza kuchukua hatua nzuri wakati alipotakiwa kuachia madaraka. Alitakiwa kuachia madaraka muda mrefu uliopita,” Chip Parirnyatwa wa Shirika la Haki za Binadamu Zimbabwe ameiambia VOA.

Badala yake Robert Mugabe ameshikilia madaraka kwa takriban miaka 40, akiendelea kukandamiza upinzani wa kisiasa na kuwafunga na kuwakandamiza wapinzani wake wa kisiasa.

Uingereza na Umoja wa Ulaya (EU) ulimwekea marufuku ya kusafiri rais baada ya vurugu za uchaguzi mwaka 2002. Mtu ambaye inaonekana amemuondoa kwenye madaraka lazima atizamwe kwa tahadhari, anahoji mchambuzi Nick Branson wa Taasisi ya Utafiti ya Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Boris Johnson amesema hali iliyopo nchini humo inahitaji kushughulikiwa kwa uangalifu.

“Hakuna mtu anataka tu kuona mabadiliko ya kuondoka kiongozi mmoja aliyekuwa hajachaguliwa anayetawala kwa mabavu kwenda mwengine, hakuna anyetaka kuona hilo. Tunataka kuona uchaguzi huru na wa haki uliosahihi mwaka ujao na hilo ndilo tutakuwa tunalitarajia.

Waziri mkuu wa uingereza ametoa hisia zake juu ya jeshi kuchukua madaraka.

Tunafuatilia maendeleo ya tukio hili kwa uangalifu, bado hali ni tete. Lakini bado tunasisitiza pande zote kuonyesha utulivu na tunawaomba nchi iepuke vurugu,” amesema kuwambia wabunge Jumatano, hisia ambazo zimeelezewa na Umoja wa Ulaya.

“Haki za msingi za raia wote lazima ziheshimiwe na amri ya kikatiba na utawala wa kidemokrasia lazima vifuatwe,” amesema msemaji wa Tume ya EU Catherine Ray.

XS
SM
MD
LG