Makombora hayo yalitumiwa Desemba 7, wizara hiyo imesema katika wimbi kubwa la mashambulizi yaliyoilenga Kyiv, na Ukraine, ya kati.
Wakati wizara ya Uingereza inasema kurushwa kwa makombora hayo mwezi Desemba huenda kulilenga kuharibu miundombinu ya nishati ya Ukraine, na ripoti za awali zinaonyesha kuwa Ukraine ilifanikiwa kuyazuia.
Uharibifu kutoka kwa makombora hayo ulikuwa mdogo kwa mujibu wa ripoti ya Uingereza, licha ya kuuwawa kwa raia mmoja katika mashambulizi.
Wakati huo huo, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, anafanya safari yake ya kwanza Amerika Kusini, alitarajiwa kuhudhuria kuapishwa kwa Javier Milei, kuwa rais mpya wa Argentina.
Forum