Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 18:27

Uingereza yaweka vikwazo watu 30 kutoka nchi 11 kwa ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu


Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza James Cleverly
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza James Cleverly

Uingereza leo Ijumaa imetangaza vikwazo vinavyolenga watu 30 duniani kote ambao imewataja kama”vigogo wa kisiasa wafisadi, wakiukaji wa haki za binadamu na wahusika wa ukatili wa kingono unaohusiana na migogoro.”

Imesema vikwazo hivyo viliratibiwa na washirika wake wa kimataifa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupambana na ufisadi na siku ya haki za binadamu duniani, na vinajumuisha watu wanaojuhusisha na vitendo viovu, ikiwemo mateso ya wafungwa na uhamasishaji wa wanajeshi kuwabaka raia.

Waziri wa mambo ya nje James Cleverly amesema katika taarifa “Leo vikwazo vyetu vinakwenda mbali zaidi kufichua wale wanaohusika na ukiukaji mbaya wa haki zetu za msingi.”

Vikwazo hivyo vinalenga watu kutoka nchi 11, wakiwemo maafisa 10 wa Iran wanaohusiana na mahakama za Iran na mifumo ya kijeshi, vigogo katika jeshi la Myanmar, Kanali wa jeshi la Russia Ibatullin kwa kuhusika kwake kama kamanda wa kikosi cha 90 cha vifaru, kundi la wanamgambo wa Mali, lijulikanalo kama Macina Liberation Front, kwa kile Uingereza imesema inahusiana na ukatili wa kingono, pamoja na maafisa wa Sudan Kusini kwa kuhusika kwao katika ukatili wa kingono.

XS
SM
MD
LG