Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 06, 2023 Local time: 08:32

Uingereza na Ufaransa wapeleka helikopta za kivita Libya


Uingereza na Ufaransa wapeleka helikopta za kivita Libya
Uingereza na Ufaransa wapeleka helikopta za kivita Libya

Mwanadiplomasia wa Marekani afanya ziara katika ngome ya waasi huko Benghazi

Uingereza na Ufaransa wameamua kupeleka helikopta zakushambulia ili kujiunga na kampeni za NATO dhidi ya majeshi ya kiongozi wa Libya Moammar Gadhafi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Alain Juppe amesema leo Jumatatu kuwa upelekaji uko katika misingi ya mamlaka ya ya Umoja wa Mataifa kuwalinda raia wa Libya. Amesema hilo litafanyika haraka iwezekanavyo.

NATO ina takriban ndege za kivita 200 kwa ajili ya operesheni zake nchini Libya, lakini haijatumia helikopta zozote kufanya mashambulizi ya kuyapiga majeshi ya Gadhafi ambayo yanawatishia raia.

Wakati huo huo, mwanadiplomasia wa juu wa Marekani yuko katika ziara ya siku tatu kwenye ngome ya waasi huko Benghazi katika kile ambacho wizara ya mambo ya nje imekiita ni ishara nyingine ya uungaji mkono wa Marekani kwa baraza la taifa la mpito la waasi. Waziri Mdogo wa Mambo ya Nje kwa masuala ya Mashariki ya Kati, Jeffrey Feltman, ni afisa mwandamizi wa marekani kuitembelea Libya tangu kuanza kwa upinzani dhidi ya Moammar Gadhafi mwezi February.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje imliita baraza la taifa la mpito ni mshiriki halali kwa ajili ya watu wa Libya.

Ziara ya mwanadiplomasia huyo imekuja siku moja baada ya mkuu wa sera za mambo ya nje katika Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton kufungua ofisi ya EU mjini Benghazi.

XS
SM
MD
LG