Msururu wa migomo unasababisha taabu kote Uingereza wakati wa kuelekea sikukuu ya Krismas huku wafanyakazi wa reli na maafisa wa kudhibiti hati za kusafiria wakitarajiwa kudumaza kipindi cha sikukuu wakati serikali imeapa kupinga madai ya nyongeza ya mishahara.
Wafanyakazi kote katika uchumi wa Uingereza wanadai ongezeko la malipo kukiwa na mfumuko wa bei ambao sasa ni takriban asilimia 11 jambo ambalo linazua mgogoro mbaya zaidi wa gharama ya maisha.
Migomo hiyo inaweka shinikizo zaidi katika utoaji wa huduma za afya kitaifa na inayofadhiliwa na serikali wakati tayari inakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi na kuwa nyuma kwa rekodi zake kutokana na ucheleweshwaji uliotokana na COVID.