Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 06:53

Wauguzi wa Uingereza waitisha mgomo wa kwanza katika historia ya miaka 106 ya chama chao


Mgomo wa wafanyakazi wa usafiri wa reli wakiomba nyongeza ya mshahara, Juni 21, 2022, Liverpool. Picha ya AFP
Mgomo wa wafanyakazi wa usafiri wa reli wakiomba nyongeza ya mshahara, Juni 21, 2022, Liverpool. Picha ya AFP

Wauguzi kote nchini Uingereza mwezi ujao wataitisha mgomo wa kwanza katika historia ya miaka 106 ya chama chao, wakiungana na wafanyakazi wengine wa Uingereza kuchukua hatua za kusimamisha kazi wakidai malipo bora.

Wafanyakazi nchini Uingereza, Wales na Ireland ya Kaskazini, lakini sio Scotland watafanya mgomo tarehe 15 na tarehe 20 Disemba, baada ya chama chao cha Royal College Nursing ( RCN) kusema kwamba serikali imepinga ombi la mashauriano.

Hii itakuwa hatua ya hivi karibuni ya kusimamisha kazi nchini Uingereza ambapo mzozo wa miongo kadhaa wa mfumuko mkubwa wa bei na gharama kubwa ya maisha, umepelekea wafanyakazi katika sekta mbalimbali kudai nyongeza ya mishahara ili kumudu kupanda kwa bei za bidhaa za msingi.

Mkurungenzi wa chama hicho cha wauguzi (RNC) Patricia Marquis leo Ijumaa amewaomba radhi wagonjwa ambao wangefanyiwa upasuaji au matibabu, na kusema kuwa “ wauguzi wamesimama ili kutetea haki zao lakini muhimu zaidi kutetea haki za wagonjwa.”

XS
SM
MD
LG