Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 21:40

Uingereza kupiga kura ya maoni Alhamis


Brexit
Brexit

Wananchi wa Uingereza wanatarajiwa kupiga kura ya maoni Alhamis ambayo itaamua iwapo nchi hiyo ijiondoe kwenye muungano wa Ulaya.

Wanaounga mkono wazo hilo walisema kuwa huu ndio wakati wa Uingereza kujikomboa na kuamua hatima ya siku zijazo. Aliekuwa meya wa London, Boris Johnson, Jumatano alipowahutubia wanaounga mkono wazo hilo mjini Essex alisema kuwa anafikiri siku ya Alhamis ni ya uhuru kwa Uingereza.

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron.

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron kwenye hotuba yake kwa taifa kupitia televisheni alisema kuwa hatua hiyo ni sawa na kuruka kutoka ndani ya ndege na kwamba uamuzi huo hauwezi kubatilishwa ukishafanyika.

Aliongeza kusema kuwa wazo kuwa Uingereza sio huru sio kweli na kwamba kujiondoa kwenye muungano huo hakutatatua tatizo lililoko la uhamiaji.

XS
SM
MD
LG