Hunt hata hivyo amesema kwamba kaya maskini hazitaongezewa kodi na kwamba hatua ya kupunguza matumizi kwa huduma za umma yatakuwa na uwiano.
Akizungumza kabla ya kutangaza mipango ya bajeti ya serikali siku ya alhamisi, Hunt alisema hakutaka kuzungumzia hali inayotarajiwa ya kudorora kwa uchumi, lakini amesema kwamba atapunguza nakisi ya bajeti ambayo imeongezeka tangu kutokea kwa janga la virusi vya Corona, na uvamizi wa kijeshi wa Russia nchini Ukraine.
Hunt na waziri mkuu Rishi Sunak wameonya kwamba watachukua maamuzi magumu sana, ili kukabiliana na mfumuko wa bei ambao umefikia asilimia 10.
Wabunge wengi wa chama kinachotawala cha Conservative wanapinga nyongeza ya kodi na huenda hatua ya serikali ya Sunak kuongeza kodi ikasababisha tena mpasuko ndani ya chama hicho.