Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 17:22

Kenya kujenga jela ya wahalifu wa kigaidi


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema serikali yake ina mipango ya kujenge jela maalum watakakozuiliwa wahalifu wa kigaidi na wale wanaowaunga mkono.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema serikali yake ina mipango ya kujenge jela maalum watakakozuiliwa wahalifu wa kigaidi na wale wanaowaunga mkono.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema serikali yake ina mipango ya kujenga jela maalum watakakozuiliwa wahalifu wa kigaidi na wale wanaowaunga mkono.

Serikali ya Kenya ina mipango ya kujenga jela mpya ya kuwashikilia washukiwa wa ugaidi na wale wanaowaunga mkono. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliyasema hayo siku ya Jumanne wakati wa sherehe za kufuzu kwa askari na maafisa wapya 2000 wa jela.

Bw. Kenyatta alisema kwamba serikali yake haitaruhusu wahalifu wa kigaidi kuvuruga Wakenya wasio na hatia yoyote wala kumruhusu yeyote kueneza uchochezi kupitia itikadi kali. Hata hivyo Kenyatta hakutoa habari Zaidi kuhusu mpango huo wa ujenzi wa jela.

Baadhi ya maafisa wa ngazi za juu katika serikali ya Kenya wameeleza wasiwasi wao kuhusu uenezaji wa itikadi kali kwa wafungwa wa kawaida, lakini pendekezo la ujenzi wa jela maalum kwa washukiwa wa ugaidi limezua maoni tofauti, hususan baina ya watetezi wa haki za kibinadamu.

Mhadhiri wa chuo kikuu cha Nairobi, Octavian Gakuru, ameiambia Sauti ya Amerika kwamba ana shaka kuhusu pendekezo hilo, kwani huenda likapelekea serikali ya Kenya kukiukahaki za binadamu.

XS
SM
MD
LG