Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 15:55

Kenyatta akutana na Kiir mjini Juba


Marais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Salva Kiir wa Sudan Kusini wazungumza na waandishi wa habari mjini Juba baada ya kufanya mazungumzo mjini Juba. Agosti 30, 2016.
Marais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Salva Kiir wa Sudan Kusini wazungumza na waandishi wa habari mjini Juba baada ya kufanya mazungumzo mjini Juba. Agosti 30, 2016.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya leo amefanya ziara ya siku moja mjini Juba, Sudan Kusini, ambako amekutana na Rais Salva Kiir katika Ikulu ya nchi hiyo, na kumshinikiza atekeleze makubaliano ya kutafuta amani yaliyotiwa saini mapema mwaka huu.

Katika taarifa iliyotolewa na ikulu ya Nairobi, Kenyatta aidha amechukua nafasi hiyo kumwelezea Kiir kwamba eneo la Afrika Mashariki na Kati linamuunga mkono katika juhudi zake za kutafuta amani.

Kutadhmini hayo, BMJ Muriithi alizungumza na naibu wa msemaji wa ikulu, Munira Mohamed, na kwanza akamuuliza ni upi hasa umuhimu wa ziara hiyo iliyofanywa na rais Kenyatta mjini Juba:

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:01 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG