Australia na New Zealand, walikuwa wenyeji wa michuano hiyo, lilikuwa kombe la dunia la wanawake la tisa na la kwanza kufanyika katika kanda ya kusini.
Licha ya mashabiki kutokuwa na hamu ya kufika uwanjani baada ya Australia kuondolewa katika duru ya nusu fainali, watu wasiopungua milioni 2 walifika uwanjani katika miji tisa wenyeji wa michezo hiyo, na zaidi ya watu 75,000 walihudhuria fainali ya leo Jumapili.
Maelfu ya mashabiki walimiminika karibu na uwanja wa michezo wa Australia mjini Sydney saa chache kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali Jumapili.
Forum