Mabati ya nyumba yalirushwa juu ya milima kutoka miji iliyo sehemu za kaskazini mashariki
Idara ya hali ya hewa ya Ufaransa imesema kimbunga Chido kilikuwa kimbunga chenye nguvu zaidi kupiga Mayotte katika muda wa zaidi ya miaka 90.
Maafisa wa Ufaransa wamesema mamia au hata maelfu ya watu huenda wamefariki kutoka na kimbunga hicho.
Kufikia sasa, watu 22 pekee wamethibitishwa kufariki.
Ni vigumu kufikia sehemu nyingi za kisiwa hicho kutokana na miundo mbinu mibovu, inayopelekea shughuli ya uokoaji kuwa ngumu.
Forum