Askofu Kakobe ametoa kauli hii Jumatatu baada ya kutoka kuhojiwa ofisi ya uhamiaji ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa takriban saa tatu.
Amesema inawezekana kuwa uhamiaji ina nia njema, lakini amehoji ni “kwa nini sasa, kwa nini wanahojiwa watu fulani wa kutoka eneo fulani la Kigoma. Mbona hatujasikia watu kutoka Dodoma, Kaskazini wakihojiwa.”
Vyanzo vya habari vimesema kuwa Askofu Kakobe ametakiwa kuacha hati yake ya kusafiria ili iweze kuwasaidia kupata taarifa zake muhimu huku yeye akisisitiza “hiki wanachokifanya kina tia shaka.”