Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 23, 2025 Local time: 10:17

Yemen yakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula


Watu wa Yemen wanasuburi kwa chakula wakati wa Ramadan.
Watu wa Yemen wanasuburi kwa chakula wakati wa Ramadan.

Raia wengi wa Yemen wanakabiliana na uhaba wa chakula kwa mujibu wa tathimini mpya ya pamoja iliyofanywa na Umoja wa Mataifa na washirika.

Tathimini ya sasa ya pamoja ya hali ya chakula “Intergrated Food Security Phase Classification" (IPC) inaonyesha kwamba kata 19 ama 22 za Yemen zinakabiliana na uhaba mkubwa wa chakula.

Taarifa zinaeleza kwamba zaidi ya nusu ya idadi ya watu nchini humo wanakabiliana na kiwango cha hatari, ikiwa ni kundi la nne katika mfumo uliogawanyishwa mara tano katika utambuzi wa hali ya uhaba wa chakula.

Uhaba wa mafuta na vikwazo vya uingizwaji ndani ya nchi vimechangia kusababisha uhaba wa chakula katika nchi iliyovitani ya Yemen.

Nchi hiyo inatumia asilimia 90 ya chakula chake kutoka nje ya nchi, na mafuta yaliyoingizwa nchini mwezi March yalitosheleza asilimia 12 tu ya mahitaji.

XS
SM
MD
LG