Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 06:43

Ugonjwa wa kisukari watabiriwa kuongezeka Afrika


Kifaa cha kitabibu cha kusoma kiwango cha sukari mwilini
Kifaa cha kitabibu cha kusoma kiwango cha sukari mwilini
Idadi ya watu wenye ugonjwa wa kisukari katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara barani Afrika inatarajiwa kuongezeka mara mbili katika kipindi cha miaka 20 ijayo. Eneo hivi sasa lina idadi kubwa ya vifo kutokana na kisukari wakati ugunduzi kamili na matibabu badi ni tatizo.

Shirikisho la kimataifa la kisukari-IDF linasema kwamba inakadiriwa watu milioni 371 hivi sasa wanaishi na kisukari ugonjwa sugu unaotokana na mwili kushindwa kutengeneza viwango vya sukari katika mfumo wa damu.

Shirika la afya duniani-WHO linasema kwamba idadi hii inaongezeka hasa katika nchi zinazoendelea ambako kumekuwepo na ongezeko la haraka katika uzito wa mwili na upungufu wa mazoezi ya viungo katika miaka ya karibuni na kusababisha aina ya pili ya kisukari.

Kama kikiachwa bila kutibiwa, kisukari kinasababisha upofu, figo kushindwa kufanya kazi, ulemavu wa viungo na hata kifo.

WHO inasema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya vifo vinavyotokana na kisukari hutokea katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati, kama vile Senegal ambako watu hawana njia mbadala za huduma ya afya au namna ya kumudu matibabu.

Nchini Senegal watu wengi wenye kisukari wanasema kwamba wana bahati kwa sababu serikali imepunguza gharama za INSULIN, dawa inayojulikana sana kutumika kutoa uwiano wa viwango vya sukari katika damu, kutoka dola 36 kwa matibabu hadi kufikia dola tatu kwa matibabu.

Hata hivyo kuna gharama kadhaa za ziada kama vile bomba la sindano, uchunguzi wa sukari mwilini, vyakula maalumu na gharama nyingine z a madawa ambazo zinaongezeka kutokana na matatizo yanayohusiana na kisukari kama vile matatizo ya mapigo ya juu ya moyo na mzunguko wa damu mwilini.

IDF inaonya kwamba kama hakuna kitu chochote kitakachofanywa ili kusitisha ukuaji wa mlipuko wa kisukari, zaidi ya mtu mmoja kati ya 10 wataathiriwa na ugonjwa huu ifikapo mwaka 2030.
XS
SM
MD
LG