Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 16:20

Sierra Leone yasema ina uwezo wa kudhibiti mlipuko wa Ebola


Mwanamke mmoja na mwanawe wakipatiwa huduma ya afya mjini Freetown, Sierra Leone
Mwanamke mmoja na mwanawe wakipatiwa huduma ya afya mjini Freetown, Sierra Leone

Wizara ya Afya ya Sierra Leone imesema wote walioachiliwa kutoka kwa karantini wametajwa na Shirika la Afya Ulimwenguni WHO ni wale ambao hawana ugonjwa huo tena.

Sierra Leone imewaachilia watu waliokuwa wamezuiliwa kwa karantini baada ya wao kupona ugonjwa wa Ebola.

Waliwekwa kwenye karantini mwezi jana baada ya visa viwili vipya vya ugonjwa huo kuripotiwa na kuthibitishwa.

Sidi Yahya Tunis, ambaye ni msemaji wa maswala ya afya ya umma kwenye wizara ya Afya nchini Sierra Leone amesema wote walioachiliwa kutoka kwa karantini wametajwa na Shirika la Afya Ulimwenguni WHO kama ambao hawana ugonjwa huo tena.

Tunis amesema kwamba kwa vyovyote vile wananchi wa Sierra Leone wanapaswa kujua kuwa sasa nchi hiyo ina uwezo wa kudhibiti au kukabiliana na visa vyovyote vipya vya virusi hivyo vya Ebola.

XS
SM
MD
LG