Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:20

Liberia yatangaza mtoto mdogo agundulika ana virusi vya Ebola


Naibu Waziri wa Afya, Tolbert Nyenswah, nchini Liberia.
Naibu Waziri wa Afya, Tolbert Nyenswah, nchini Liberia.

Maafisa wa Afya nchini Liberia wanasema mtoto mmoja wa miaka mitano amekutwa na virusi vya Ebiola siku chache baada ya mama yake kufariki dunia na ugonjwa huo.

Mwanamke mmoja wa mwenye umri wa miaka 30 alifariki kutokana na Ebola wiki iliyopita mjini Monrovia miezi kadhaa baada ya Liberia kutangazwa haina ugonjwa huo tena.

Kifo chake kilifuatia mlipuko wa hivi karibuni ambao uliuwa watu wanne katika nchi jirani ya Guinea.

Naibu Waziri wa Afya Tolbert Nyenswah, ambaye pia ndiye mkuu wa kitengo cha usimamizi wa matukio ya dharura, amesema mlipuko wa hivi karibuni ulitokea Guinea. Lakini akasema tofauti na siku za nyuma mfumo wa afya Liberia unaweza kudhibiti mlipuko huo.

XS
SM
MD
LG