Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 07:55

Uganda yasherehekea miaka 26 ya chama tawala.


Rais wa Uganda Yoweri Museveni, kulia akisalimiana na Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni, kulia akisalimiana na Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Sherehe za kuadhimisha siku hii zilifanyika wilayani Kapchorwa kilomita 300 mashariki mwa Uganda.

Uganda Alhamisi imesherehekea miaka 26 ya ushindi wa chama tawala cha NRM. Tarehe 25 Januari mwaka wa 1986, Rais Yoweri Museveni akishirikiana na wanajeshi 27 wa jeshi lake la National Resistance Army - NRA, waliuteka nyara mji mkuu wa Uganda - Kampala na kuung'oa mamlakani utawala wa kijeshi wa Tito Okello Lutwa.

Sherehe za kuadhimisha siku hii zilifanyika wilayani Kapchorwa kilomita 300 mashariki mwa Uganda. Miongoni mwa waliohudhuria na kutunukiwa kwa mchango wao wakati wa vita vya msituni ni rais wa Rwanda Paul Kagame rais na wa Equitoria Guinea ambaye pia ni mwenyekiti wa umoja wa Afrika-Theodore Nguema.



Jeshi la National Resistance Army (NRA) lililoongozwa na rais Yoweri Museveni lilikuwa msituni kwa miaka mitano kuanzia 1981-1986 likipinga utawala wa Milton Obote na kisha kiongozi wa kijeshi Tito Okello Lutwa.

Januari 26 mwaka wa 1986, Rais Museveni aliapishwa kuwa rais wa Uganda.

Baadhi ya mabadiliko ambayo Serikali yake inajivunia ni amani na usalama, uchumi bora, uhuru wa kusema, uzalishaji wa umeme na ujenzi wa barabara bora.

Rais Yoweri Museveni alimtunukia rais wa Rwanda Paul Kagame kwa mchango wake wakiwa msituni kwenye vita vilivyoitwa vya Luweero.

Rais Kagame alikuja Uganda akiwa na umri wa miaka miwili mwaka wa 1960. Aliishi Uganda kwa miaka thelathini. Mwaka wa 1981 akajiunga na jeshi la NRA lengo likiwa kumng'oa madarakani Milton Obote.

Rais Kagame kando na kupigana bega kwa bega na Rais Museveni, alikuwa afisa wa ujasusi.

Rais Kagame alipewa medali tatu. Ile ya Lulu ya Afrika, ya kagera na ya Luweero triangle kwa sababu alikuwa miongoni mwa wapiganaji ishirini na saba walioingia mjini Kampala tarehe ishirini na tano januari ya mwaka wa 1986 na kumng’oa mamlakani kiongozi wa kijeshi Tito Okello Lutwa.

Rais wa Eguitoria Guinea Theodore Obiang Nguema mwenye umri wa miaka sabini na ambaye amekuwa rais kwa miaka 33 hakuondoka mikono mitupu. Naye pia alitunukiwa medali ya lulu ya Afrika.

Medali hii ya Lulu ya afrika hupewa marais ambao wanatambuliwa na serikali ya Uganda kama wakombozi ambao walichangia kuleta mabadiliko nchini Uganda au nchini mwao.

XS
SM
MD
LG